Barbara akerwa na uwanja wa Plateau United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Nov 2020
Barbara akerwa na uwanja wa Plateau United

Pamoja na kuwapongeza wachezaji wa Simba kwa kupambana na kufanikiwa kuwapa furaha Wanamsimbazi na Watanzania kwa ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Plateau United nchini Nigeria, Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amehoji vigezo vilivyotumiwa na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kuidhinisha uwanja wa New Jos kutumiwa katika michuano ya ligi ya mabingwa

"Nawapongeza wachezaji wamepambana katika mazingira magumu. Tumepata ushindi muhimu ambao tunakwenda kuulinda mchezo wa marudiano Dar es salaam kuhakikisha tunasonga mbele hatua inayofuata."

"Ningeliomba Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupitia upya vigezo vilivyotumika kuruhusu mchezo wetu kuchezwa kwenye dimba la New Jos ilihali uwanja huo haujakidhi viwango vinavyohitajika," alisema Barbara

Bao la Clatous Chama limeihakikishia Simba ushindi muhimu ambao utawaongezea morali kuhakikisha wanamaliza kazi kwenye wa marudiano ambao utapigwa jijini Dar es salaam Jumamosi, Disemba 05

Simba tayari imeondoka nchini Nigeria ikitarajiwa kuwasili nchini kesho Jumanne majira ya saa kumi Alasiri

Watatua uwanja wa Ndege wa KIA kisha kuunganisha moja kwa moja jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’