Simba imepambana kiume kuondoka na alama zote tatu nchini Nigeria wakiwachapa Plateau United bao 1-0
Ulikuwa mchezo mgumu uliogubikwa na matukio mengi ya nje ya uwanja
Ushindi katika mazingira hayo haukuwa rahisi, lakini kwa hakika Simba imedhihirisha iko imara
Wameanza kwa ushindi kama walivyofanya misimu miwili iliyopita, mwanzo huu ni dalili njema




Kocha Sven Vandenbroeck hapaswi kubweteka na ushindi huu, mchezo wa marudiano jijini Dar es salaam Simba itahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare
Mchezo huo pia utashuhudiwa na takribani mashabiki 30,000 ambao watawaongezea hamasa wachezaji
Simba ina nafasi nyingine ya kwenda makundi msimu huu kwani kama itavuka hatua hii ya awali, huenda ikakutana na Platinum Fc ya Zimbabwe kwenye mchezo wa raundi ya kwanza
Platinum nao walishinda mabao 2-1 ugenini hapo jana