Simba imeunguruma viunga vya ugenini nchini Nigeria baada ya kuichapa Plateau United bao 1-0 katika mchezo mgumu uliopigwa uwanja wa New Jos
Clatous Chotta Chama 'CCC' mchezaji wa mechi kubwa, ameendeleza rekodi yake ya kufunga mabao muhimu leo akiweka kambani bao pekee la Simba ambalo linawafanya warudi nyumbani wakiwa na faida ya ushindi na bao moja la ugenini
Mpango wa mchezo wa kocha Sven Vandenbroeck ulifanikiwa leo, Simba ikiwa makini sana katika ulinzi lakini kongole nyingi akistahili mlinda lango Aishi Manula aiyekuwa bora sana leo
Pamoja na figisu nyingi za Plateau United, wametandikwa hapo hapo kwenye uwanja wao
Sasa shughuli wanayo wakija jijini Dar es salaam
Ndio kwanza msimu wa ligi ya mabingwa umeanza, hii ndio Simba sasa...!
ADVERTISE HERE