Msafara wa kikosi cha Simba ukiwa na watu 43, wachezaji, benchi la ufundi na viongozi walipimwa vmaambukizi ya COVID-19 na habari jema ni kuwa hakuna aliyekutwa na maambukizi ya corona
Kwa maana hiyo Kocha Sven Vandenbroeck ana uhakika wa kumtumia mchezaji yeyote miongoni mwa wachezaji wake 24 kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Plateau United ambao utapigwa baadae leo huko Nigeria
Kulikuwa na taarifa ya kuwepo mpango ovu wa kutumia vipimo vya corona kuwakwamisha baadhi ya wachezaji muhimu wa Simba kushiriki mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 12 jioni
Uongozi wa Simba umethibitisha kuwa hakuna aliyekutwa na corona hivyo kila mchezaji yuko tayari kwa mchezo huo ambao hata hivyo Watanzania hawataweza kuuona mbashara baada ya maafisa wa Plateau United kugoma kutoa haki za matangazo kwa Azam TV