Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo wanaanza kampeni ya msimu mpya wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika wakiwa ugenini Nigeria dhidi ya mabingwa wenzao wa nchi hiyo Plateau United
Mchezo utapigwa kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Tanzania wakati kule Nigeria itakuwa saa kumi Alasiri
Mazingira ya mchezo huo tayari yamefanywa kuwa magumu na wenyeji Plateau United ambao jana walizuia mchezo huo kuonyeshwa mbashara na televisheni
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo na watacheza kwa tahadhari kubwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri
Mabingwa hao wa Tanzania wakiwa na kumbukumbu ya kutolewa hatua ya awali kwenye michuano iliyopita, msimu huu hawatapenda kuona jambo hilo linajirudia
Mashabiki wa Simba na wadau wote wa soka nchini dua zao ni kwa Simba ili iweze kufanya vizuri kwenye mchezo huo
Ni kwa sababu mafanikio ya Simba ni mafanikio ya nchi
Kila la kheri Simba Sc, Kila la kheri Machampioni wa Taifa hili