Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, Namungo Fc wameanza vyema kampeni ya michuano hiyo baada ya kuichapa Al Ratiba kutoka Sudan Kusini kwa mabao 3-0
Mabao mawili ya Steven Ssey na moja la Shiza Kichuya yalitosha kuihakikishia Namungo Fc ushindi muhimu ambao umewaweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele hatua inayofuata
Mchezo wa marudiano utapigwa wiki ijayo huko Sudan Kusini
Wawakilishi wa Nchi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Simba wao wako nchini Nigeria wakitarajiwa kushuka dimbani kesho Jumapili kuikabili Plateau United
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amesema Watanzania wote wanapaswa kuiombea Simba ili iweze kufanya vizuri katika michuano hii ya vilabu bingwa barani Afrika
Amesema mafanikio ya Simba ni mafanikio ya Tanzania
"Kesho ndo siku ambayo Mabingwa wa Nchi tunaanza safari kama Wawakilishi pekee katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika. Hivyo basi, kila mmoja wetu kwa anachokiamini tufanye dua na kuiombea Simba iweze kufanya vizuri. Simba ikifanya vizuri sio kwa maslahi ya WanaSimba peke yake bali kwa Watanzania wote kwa ujumla"