Tuko tayari kuikabili Plateau United - Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Nov 2020
Tuko tayari kuikabili Plateau United - Sven

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema amekamilisha maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Plateau United ambao utapigwa kesho Jumapili uwanja wa New Jos, Nigeria

Sven amesema vijana wake wako timamu kimwili na kiakil, kila mmoja akiwa tayari kuelekea mchezo huo

Amesema kama timu wameweka malengo ya kupata matokeo mazuri ambayo yatawaweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele hatua inayofuata

"Kila kitu kipo sawa, kila mmoja yupo tayari kwa mchezo na wana furaha na hilo. Tulichofanyia kazi wiki kadhaa zilizopita inabidi tukitumie kesho. Mipango yetu imejikita zaidi upande wetu ili kuhakikisha tunapata ushindi"

"Hatuna taarifa kuhusu Plateau United lakini mwanzoni tutaanza kwa kuimarisha eneo la ulinzi na kuangalia uimara na udhaifu wao upo eneo gani na baada ya hapo tutaangalia cha kufanya," alisema Sven

Nao wachezaji nahodha John Bocco na Clatous Chama wamewaahidi Wanamsimbazi kuwa kesho watakuwa na kazi moja tu, kuipigania timu kuhakikisha wanapata matokeo mazuri

"Tunajua wamejiandaa lakini sisi tunaenda kupambana kwa ajili ya timu yetu ili tushinde na kupata matokeo mazuri," alisema Bocco

"Tunatakiwa kuwa makini na tufanye kazi kwa pamoja. Tunaamini tunauwezo wa kufika mbali zaidi huu msimu. Hii mechi tunategemea matokeo mazuri kuanzia hapa Nigeria na tukipata matokeo hapa itakuwa rahisi kumalizia kule Tanzania," maneno ya Clatous Chama

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’