Simba yapotezea hujuma Nigeria

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Nov 2020
Simba yapotezea hujuma Nigeria

Mratibu wa Simba Abbas Gaza amesema kikosi kiliwasili salama Mjini Jos wakiendelea na maandalizi yao kuelekea mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Plateau United

Mchezo utapigwa kesho Jumapili saa kumi Alasiri kwa saa za Nigeria ambapo kwetu Tanzania itakuwa saa 12 jioni

Kumekuwa na matukio ya hapa na pale ambayo Simba imekutana nayo, hata hivyo mabingwa hao wa nchi walijipanga kukabiliana na mazingira yoyote ugenini kwani kwa soka la Afrika mambo hayo ni jambo la kawaida

Katika moja ya changamoto ambazo Simba walikumbana nayo jana baada ya kuwasili mji wa Jos ni pale wapishi wa Simba walipokataliwa  kupika chakula katika Hoteli waliyofikia, wenye hotel wakigoma na kusisitiza chakula lazima kipikwe na wapishi wao

Lakini pia kumekuwa na taarifa ya uwepo wa mpango wa kuwakwamisha baadhi ya wachezaji wa Simba wasishiriki mchezo huo kwa kisingizio cha vipimo vya COVID-19

Juzi walizusha taarifa za kudai kunasa mpango wa baadhi ya wachezaji wa Plateau United kuhongwa na maafisa wa Simba, jambo ambalo halikuwana ukweli wowote

Plateau United ni kama wameingia hofu baada ya kubaini Simba iko imara na zaidi mafanikio iliyopata Simba katika michuano hiyo misimu miwili iliyopita

Gaza amesema hawatishwi na changamoto wanazokutana nazo kwani walizitarajia lakini muhimu kwao ni kuhakikisha wanapambana ili kupata matokeo

"Kila kitu kinakwenda kwa namna ambavyo kimepangwa, hatuna mashaka tunaamini kwamba yote ambayo yanatokeo huku tutapambana kupata matokeo," alisema

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’