Wababe wa soka barani Afrika, Al Ahly wameendeleza umwamba wao usiku wa kuamkia leo wakitwaa taji la tisa la ligi ya mabingwa baada ya kuwafunga mahasimu wao Zamalek katika mchezo wa fainali
Ratiba ya Michuano ya ligi ya mabingwa iliathiriwa na korona hivyo kupelekea michuano hiyo ya msimu uliopita kuhitimishwa jana wakati michuano ya msimu huu ikitarajiwa kuanza leo
Al Ahly waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo ambao ulikosa shamrashamra za mashabiki
Mkufunzi wa Al Ahly Pitso Masemane, ameingia kwenye rekodi ya kutwaa taji la ligi ya mabingwa akiwa na vilabu viwili tofauti
Alitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza akiwa na Mamelodi Sundowns akiwafunga Zamaleki. Jana akarudia tena akiwa na Al Ahly pia akiwafunga Zamaleki
Kampeni ya michuano ya msimu mpya inaanza leo kwa mechi za hatua ya awali kupigwa
Mabingwa wa Tanzania Bara Simba wao watashuka dimbani nchini Nigeria hapo kesho katika mchezo dhidi ya Plateau United