Baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Gendarmerie jana kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre amesema sasa wanajipanga kumaliza kazi kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa February 20, 2018.
Lechantre amesema ushindi huo mnono umewaweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Nae kocha Msaidizi Masudi Djuma amesema ameridhika na ushindi iliyopata Simba jana japo alitamani ushindi mnono zaidi kutokana na nafasi nyingi ilizotengeneza.
“Tunashukuru tumeanza vizuri kwa ushindi wa magoli manne, tulitengeneza nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia lakini tunajua ni mchezo tu cha msingi washambuliaji wetu wawili wote wamefunga.†amesema Djuma.
Simba inajiandaa kuivaa Mwadui FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Alhamisi, February 15, mchezo utakaopigwa mkoani Shinyanga kabla ya kuifuata Gendarmerie huko Djibouti kwa mchezo wa marudiano

ADVERTISE HERE