Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amemshauri kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck kuhakikisha anakwenda katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Plateau United ya Nigeria kwa tahadha
Simba itashuka dimbani Jumapili kuvaana na Plateau United katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utapigwa saa 12 jioni uwanja wa New Jos
Pamoja na kutambia rekodi nzuri ya klabu ya Simba kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, Rage amesema timu za Nigeria zimekuwa na kawaida ya kuipa changamoto Simba kila mabingwa hao wa nchi wanapokutana nao

"Sina matatizo na Simba katika michuano hii ya ligi ya mabingwa kwani tuna rekodi nzuri huko nyuma, sisi ndio timu ya kwanza kutwaa Kombe la Cecafa mwaka 1974, pia mwaka huohuo tulifanikiwa kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufika nusu fainali ya klabu Bingwa Afrika katika ukanda wetu, hivyo sina shida nayo"
"Lakini kocha anatakiwa kwenda kwa tahadhari kubwa kuelekea mchezo huo kwani tuna historia mbaya na timu za Nigeria kila tukipangiwa kwani tumekuwa hatuvuki mbele yao, hivyo wanahitaji kuwa na maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo"
"Nina imani, safari hii jinsi kikosi kilivyo, tutafanikiwa kuvuka, kikosi kipo vizuri," alisema Rage"