Uongozi wa Simba umeeleza kupokelewa vizuri nchini Nigeria na watahakikisha timu inakuwa katika usalama muda wote
Ulinzi kwenye kambi ya Simba umeimarishwa kutokana na hali ya usalama wa nchi hiyo
Kikosi cha mabingwa hao wa nchi kiliwasili nchini Nigeria jana. Mratibu wa Simba, Abas Ally alitangulia mapema kuweka mipango sawa.
Mratibu huyo amesema kuwa mazingira ya Nigeria ni mazuri na alipata ushirikiano mkubwa kutoka chama cha soka cha nchini Nigeria.
Aliongeza kuwa usalama wa hali ya Jos inaeleweka kuwa haipo sawa kwa wageni ambao wanafika ila kwa wenyeji wao wanaona kila kitu kinakwenda sawa
Taarifa iliyotolewa na Simba mapema leo ilieleza kuwa kikosi leo kitaanza rasmi mazoezi AbujaΒ kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Plateau FC ambao utapigwa siku ya jumapili, Novemba 29, 2020 kwenye uwanja wa New Jos uliopo mji wa Jos kuanzia saa 10:00 jioni (saa 12:00 jioni - Tanzania)
Mapema leo, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dk Benson Bana alitembelea kambi ya klabu ya Simba iliyoko Abuja

