Mabingwa wa nchi Simba walitua nchini Nigeria jana tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Plateau United ambao utapigwa mwishoni mwa wiki
Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck ameamua kuweka kambi ya muda mfupi jiji la Abuja kukamilisha maandalizi yake kabla ya kusogea mji wa Jos ambako ndiko mchezo dhidi ya Plateau utapigwa
Simba ilianza maandalizi yake jana jioni, leo wanatarajiwa kuendelea na maandalizi lengo likiwa kuhakikisha hawapotezi mchezo huo wa ugenini
Kikosi cha wachezaji 24 watakuwa na kazi ya kuhakikisha wanawapa furaha Wanamsimbazi na kuipa nchi heshima kwa mara nyingine kama walivyofanya misimu miwili iliyopita
ADVERTISE HERE