Leo dunia inaomboleza kifo cha gwiji wa soka duniani Diego Armando Maradona ambaye amefariki dunia kutokqna na shambulizi la moyo
Kwa wafuatiliaji wa soka duniani, jina la Maradona haliwezi kuwa geni masikioni mwao
Pamoja na kuwa alitamba miaka ya 80, Maradona raia wa Argentina anatajwa kuwa mchezaji bora zaidi duniani akiwa kwenye ligi moja ya ushindani na Pele kutoka Brazil
Wakati akiwa klabu ya Napoli ya nchini Italia, Maradona alipata umaarufu zaidi baada ya kuisaidia timu hiyo kutoka chini na kuwa mabingwa wa Italia mara mbili
Maradona pia alishinda kombe la dunia mwaka 1986 akikumbukwa kwa bao lake alilofunga kwa mkono kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani
Pamoja na changamoto zake nyingi za nje ya uwanja hasa matumizi ya mihadarati, Maradona alikuwa na kipaji cha kusakata kabumbu
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 60
Buriani Maradona, buriani gwiji la soka