Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ameeleza kuridhia kumaliza tofauti zake na Mbunge, Mwanachama wa klabu ya Simba Hamis Kigwangallah ambaye hivi karibuni aliomba radhi kutokana na sintofahamu iliyojitokeza kati yake na Mo
Mo amesema tofauti zilizotokea kati yao, zilisukumwa na nia njema walizokuwa nazo katika kuhitaji maendeleo ya klabu
Amesema ni wakati wana Simba kuwa wamoja kuhakikisha wanashirikiana kujenga Simba imara

"Nia njema ni tabibu, nia njema ni ibada. Sote tuna mapenzi ya dhati na Simba, hata tulipokwazana ilikua katika nia njema kwenye maendeleo ya timu yetu. Naomba radhi nilipokosea na mimi uliponikosea nishasamehe. Tuijenge Simba pamoja sasa," aliandika Mo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Simba wakati huu iko angani ikielekea nchini Nigeria ambako mwishoni mwa wiki wanakabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Plateau United