Wekundu wa Msimbazi, Simba wameanza kwa kishindo kampeni ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuilaza Gendermerie ya Djibouti mabao 4-0 kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Simba ilitawala mchezo huo tangu dakika ya kwanza na ilifunga bao la kuongoza katika dakika hiyo hiyo baada ya mpira wa adhabu uliopigwa kifundi na Said Hamisi Ndemla kutumbukia kimiani.
Dalili za mvua ya mabao kuinyemelea Gendarmarie zilionekana mapema kwani kasi ya mashambulizi ya Simba iliwapa wakati mgumu vijana hao.
Mabao mengine ya Simba yalifungwa na nahodha John Bocco aliyefunga mabao mawili kupitia mipira ya kichwa kwenye dakika za 31 na 45 huku pacha wake Emanuel Okwi akiifungia Simba bao la nne kwenye dakika za majeruhi kupitia mpira wa adhabu aliosetiwa na Erasto Nyoni

Nafasi pekee ya wazi waliyokosa Gendermarie ni mkwaju wa penati waliopewa kwenye dakika ya 50, baada ya mlinzi Erasto Nyoni kumfanyia madhambi mshambuliaji wao.
Hata hivyo Aishi Manula aliokoa penati hiyo.

Kwa tathmini rahisi tu ni kwamba Simba itaenda kukamilisha ratiba tu kwenye mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa wiki ijayo, Februari 20.
Kwa kiwango chake na uwezo wake mkubwa, ni muujiza pekee utaiwezesha Gendarmerie kurejesha mabao manne kwenye dimba lao huko Djibouti.
Zaidi Wa Djibout hao wataoga mabao mengi kwenye mchezo wa marudiano!
Hakika mnyama amerejea katika michuano ya Kimataifa kwa kishindo kikuu.

ADVERTISE HERE