Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amefunguka sababu ya kutomjumuisha kikosini kiungo Jonas Mkude 'Nungunungu' kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao ulipigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid juzi na Simba kuondoka na ushindi wa mabao 7-0
Wakati Meddie Kagere na Luis Miquissone wakichelewa kurejea nchini kutoka katika majukumu ya timu za Taifa, Mkude yeye alichelewa kuripoti kambini
Akizungumza baada ya mchezo, Sven alisema Mkude hakumjumuisha katika timu ikiwa ni sehemu ya adhabu yake baada ya kuchelewa kuingia kambini
Hata hivyo nyota huyo tayari amerejeshwa kikosini kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Plateau United ambao utapigwa mwishoni mwa wiki nchini Nigeria
Mara kwa mara Mkude amejikuta matatani na makocha tofauti kutokana na utamaduni wake wa kuchelewa pale anapoitwa timu ya Taifa au kuchelewa kurudi anapomaliza majukumu ya timu ya Taifa