FT : Coastal Union 0-7 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Nov 2020
FT : Coastal Union 0-7 Simba

Kipigo kingine cha mbwa koko kimeiangukia Coastal Union leo baada ya kukubali kichapo cha mabao 7-0 kutoka kwa mabingwa wa nchi, Simba

Ulikuwa mchezo wa ligi kuu ambao ulipigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha ukishuhudiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez akiwa sambamba na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi

Ubora wa Simba ulidhihiri mapema tu kwani walihitaji dakika tatu kuandika bao la kuongoza kupitia kwa Hassan Dilunga

Mvua ya mabao ikafuatia, nahodha John Bocco akiwa mchezaji wa pili kufunga hat-trik msimu huu

Winga Bernard Morrison naye akafungua akaunti yake ya mabao, akiweka kambani bao kwa ustadi kabisa dakika za lala salama kipindi cha kwanza

Kipindi cha pili Simba iliendelea kutawala mchezo, kilichokuwa kikisubiriwa  ni idadi ya mabao yatakayopatikana kwenye kipindi hicho

Mwamba wa Lusaka Clatous Chama akaongeza mawili na hivyo kuihakikishia Simba ushindi huo mnono

Simba hii, sio ya kuisogelea hasa inapokuwa kwenye ubora wake, Coastal Union walijaribu kupimana ubavu na maji yenye kina kirefu, wakazama!

Hiki ni kipigo cha pili kikubwa Simba inaishushia Coastal Union, msimu mmoja nyuma, wagosi wa kaya walivurumishwa mabao 8-0 pale uwanja wa Uhuru

Ushindi huu ni salamu kwa Plateau United ambao ndio wanaofuata kuonja machngu ya Mnyama kwenye mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa ambao utapigwa wiki ijayo nchini Nigeria

Mchezo wa marudiano utapigwa nchini mwanzoni mwa mwezi Disemba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’