Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo wako ugenini mkoani Arusha majira ya saa kumi jioni wakitarajiwa kushuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuikabili Coastal Union
Baada ya mapumziko ya mechi za kuwania kufuzu Afcon 2021, ligi imerejea kuanzia mzunguuko wa 12
Simba mabingwa mara tatu mfululizo, wamejipanga kutetea taji lao kwa msimu wa nne na katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, mkakati uliopo ni kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kabla ya duru ya kwanza kumalizika
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa kumi Alasiri
Aidha Sven amebainisha kuwa baadhi ya wachezaji watakosekana leo akiwataja Jonas Mkude, Luis Miquissone, Meddie Kagere na Chris Mugalu
Huu utakuwa mchezo wa pili Simba inacheza uwanja wa Sheikh Amri Abeid msimu huu
Mapema kabla ya msimu kuanza, walishinda Ngao ya Jamii kwenye uwanja huo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo Fc
Kila la kheri Mnyama....!