Matukio ya rushwa kwenye soka hayakubaliki - Mo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Nov 2020
Matukio ya rushwa kwenye soka hayakubaliki - Mo

Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo', amesema endapo rushwa michezoni 'itafumbiwa macho', soka la Tanzania halitaendelea

Mo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, juzi alialikwa kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na wanachama wa Simba wa Tawi la Bunge ‘Simba Mjengoni’, yenye lengo la kukutana na viongozi mbalimbali wa timu hiyo.

"Tabia ya rushwa michezoni, kununua waamuzi na hujuma haviwezi kuendeleza soka letu, mageuzi katika mifumo wa uendelezaji wa vilabu vyetu ndio jawabu, maana klabu zetu lazima zizaliwe upya kama inavyofanya Simba ili soka letu liende mbele na la Tanzania pia,” alisema Mo.

Mwenyekiti huyo alisema klabu hiyo ina mpango wa kuwa na timu za vijana za umri chini ya miaka 18, 17, 16 na 15 na wanatarajia kuzunguka kila mkoa ili kusaka vipaji hivyo.

"Tunaenda mkoa kwa mkoa kusaka vipaji, tutawaleta na kuwasomesha na kutafuta familia ya kukaa nao ili kuwajenga kinidhamu, kidini,” alisema mwekezaji huyo.

Aidha, Mo aliwatoa hofu wanachama na mashabiki juu ya uwekezaji wake wa Sh. bilioni 20 na kueleza mambo yatakapokuwa sawa, watafikia tamati ya mjadala huo.

"Napenda kuwatoa hofu kuhusu Sh. bilioni 20, hakuna haja ya kuwa na hofu. Simba kwangu sio biashara bali ni familia kwanza. Mapenzi yangu kwa Simba hayapimiki kwa fedha. Matamanio yangu ni Simba kufanikiwa kimataifa,"aliongeza.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’