Wakala wa kiungo Clatous Chama amethibitisha kuwa mteja wake ataendelea kubaki Msimbazi mpaka mwaka 2023 baada ya kuongeza mkataba wa miaka miwili
Baada ya sintofahamu ya wiki kadhaa kuhusu hatma yake, sasa mjadala wake umefungwa kibabe na Bosi Bilionea Mohammed Dewji 'Mo'
Chama amepewa mkataba mnono ambao utamfanya awe mchezaji ghali zaidi nchini
Kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki, Simba ndio klabu inayolipa wachezaji wake mishahara minono
Ilikuwa jambo la kushangaza mwamba huyu kutoka jiji la Lusaka kuhusishwa na klabu ya Yanga ambayo kila mmoja anafahamu hali yao kiuchumi, GSM wanaokoa jahazi tu!
Kwa sasa ni wazi hakuna mchezaji anaweza kuondoka Simba na kwenda kujiunga na timu nyingine katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, labda aachwe na Simba
Huku Simba hakuna maneno mengi, ni mwendo wa kufunga watu midomo kwa vitendo tu...!