Tuna nafasi ya kufuzu Afcon - Manula

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Nov 2020
Tuna nafasi ya kufuzu Afcon - Manula

Mlinda lango namba moja wa timu ya Taifa Aishi Manula amesema anaamini bado wana nafasi ya kufuzu fainali za michuano ya Afcon 2021 itakayofanyika mwakani nchini Cameroon

Manula alikuwa sehemu ya kikosi cha Stars ambacho jana kililazimishwa matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia

Mlinda lango huyo bora Tanzania kwa misimu minne mfululizo, amesema umoja na mshikamano ndio silaha muhimu katika kampeni ya kusaka nafasi hiyo

"Bado kama nchi tuna nafasi ya kufuzu kwenda AFCON, umoja na mshikamano kama nchi ni bora na muhimu zaidi kwa sasa kwenye michezo iliyobaki, tutarejea tukiwa imara na kupata tiketi ya kufuzu inshaallah," aliandika Manula kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Stars haipaswi kupoteza mchezo katika miwili iliyobaki ili kuwa na nafasi ya kufuzu

Katika msimamo wa kundi J inashika nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia alama nne, Guinea ya Ikweta iko juu yake nafasi ya pili ikiwa na alama sita

Tunisia tayari imefuzu ikiwa vinara wa kundi J na alama zao 10 wakati Libya inashika nafasi ya nne ikiwa na alama tatu

Michezo ya kukamilisha hatua ya makundi itapigwa mwakani ambapo Stars itaanzia ugenini kuikabili Guinea ya Ikweta kisha kurejea nchini kumaliza mchezo wa mwisho dhidi ya Libya

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’