Nahodha wa Simba John Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom kwa mwezi Januari 2018.
Bocco ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba na Awesu Awesu wa Mwadui.
Bocco alitoa mchango mkubwa kwa Simba mwezi huo ikipata pointi tisa katika michezo mitatu iliyocheza na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi, huku mshambuliaji huyo akifunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za usaidizi wa bao.
Bocco atazawadiwa tuzo, kisimbuzi cha Azam na fedha taslimu sh. milioni moja kutoka kwa Mdhamini Mkuu wa Ligi, Kampuni ya Vodacom Tanzania.
Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu na miezi yao katika mabano ni Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).
Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba) na mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Disemba)

ADVERTISE HERE