Stars uso kwa uso dhidi ya Tunisia leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Nov 2020
Stars uso kwa uso dhidi ya Tunisia leo

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo wana kazi moja tu, kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu dhidi ya Tunisia katika mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya fainali za Afcon 2021

Huu ni mchezo wa kufa au kupona kwa Stars kwani ni alama tatu ndizo zitakazowaweka katika mbio za kuwania kufuzu tiketi ya michuano hiyo kwa mara ya tatu

Ushindani ni mkali kwani ukiiacha Tunisia ambayo iko kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kundi J ikiwa na alama tisa, Tanzania, Guinea ya Ikweta na Libya zina alama tatu kila moja

Matokeo tofauti na ushindi yanaweza kukatisha matumaini ya kufuzu kwa michuano hiyo

Kocha Etienne Ndayiragije amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo, jana wakikamilisha maandalizi ya mwisho

Ndayiragije amesema ni mchezaji mmoja tu Salum Abubakar ambaye atakosekana kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo uliopita

Tunisia wao hawatakuwa na presha sana leo kwani kimahesabu, wanahitaji alama moja kutoka mechi tatu zilizobaki waweze kufuzu

Mashabiki wa soka nchini wametakiwa kuwa wamoja kwa kuiunga mkono timu ya taifa ili iweze kuibuka na ushindi

Mechi itapigwa kuanzia saa nne usiku yakiwa ni maelekezo ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF)

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’