Mo atenga Mamilioni Ligi ya Mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Nov 2020
Mo atenga Mamilioni Ligi ya Mabingwa

Mabingwa wa nchi Simba hawana presha yoyote kuelekea michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambayo hatua ya awali inaanza mwishoni mwa mwezi huu. Bajeti kabambe ya fedha imetengwa kwa ajili ya kuiandaa timu kuelekea michuano hiyo

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ bila kuitaja, alisema bajeti hiyo ni kubwa na haihusiani na michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Shabaha yetu ni kufanya vyema kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika safari hii, ili kufika huko tumetenga bajeti inayojitegemea sambamba na motisha watakayopewa wachezaji watakapofanya vizuri katika mechi hizo, " alisema Dewji.

Dewji alisema baada ya kuwajua mpinzani wao, sasa wanajipanga upya wakijua changamoto gani walizopata msimu uliopita na kutolewa katika raundi ya mwanzo kabisa.

"Tumeshamjua mshindani wetu, tunaenda katika mashindano tukiwa na rekodi mbaya ya kutolewa mapema msimu uliopita na UD Songo ya Msumbiji, sasa tunajipanga vizuri kuwakilisha nchi vizuri," alisema Dewji.

Alisema wanaenda kuanzia ugenini wakiwa na faida ya wenyeji kucheza mchezo huo wakiwa bila mashabiki wao kutokana na ugonjwa wa covid-19 hali ambayo itapunguza presha kwa wachezaji wa Simba.

"Na tukaporudi kucheza nyumbani taarifa njema ni kwamba mashabiki wataruhusiwa kuingia nusu ya uwanja, hii itakuwa faida kwetu kwani tutakuwa nyumbani hivyo ni fursa kwetu kupigania ushindi," alisema.

Pia alisema wana mpango wa kuandika barua kwenda Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuomba waruhusiwe kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni watatu kuwatumia kwenye michuano hiyo.

"Kuelekea kwenye dirisha dogo tutafanya usajili wa wachezaji baada ya Gerson Fraga kuumia na tunataka mchezaji wa kumbadili, lakini pia tutaandika barua kwenda TFF kuomba kuongeza wachezaji zaidi ya 10 ili kuwatumia katika michezo ya kimataifa," alisema.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
50m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’