Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji amesema kuanzia sasa hakuna Mjumbe wa Bodi hiyo atazungumza na Wanahabari pasipo kupewa ruhusa na Mwenyekiti
Kauli ya hivi karibuni ya Mjumbe wa Bodi Zacharia Hanspoppe baada ya mchezo dhidi ya Yanga uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1, ilizua sintofahamu baada ya kuwatuhumu baadhi ya wachezaji kucheza chini ya kiwango
Akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayoihusu klabu ya Simba mapema leo, Mo amesema sasa wameweka utaratibi mzuri ambao utaepusha kujitokeza kwa matukio ya aina hiyo
"Tumekubaliana kwamba hakuna Mwanabodi ataruhusiwa kuongea na vyombo vya habari kuhusu mambo ya klabu, Hans Pope hatongea tena bila ruhusa ya Mwenyekiti na mimi nikimruhusu tutakubaliana aongee nini, kwahiyo aliyoongea tuachane nayo," alisema Mo