Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji amesema mkakati walionao wakati dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa ni kuongeza angalau wachezaji wanne na pia wapo watakaoachwa
Mo amesema miongoni mwa wachezaji watakaoachwa ni kiungo raia wa Brazil Gerson Fraga ambaye alipata majeraha yatakayomuweka nje kwa muda mrefu
Aidha kuhusu usajili wa CAF, Mo amesema wanasubiri mwongozo wa TFF kwani CAF imewaruhusu kuongeza wachezaji 10
"Fraga ameumia na atakuwa nje kwa muda mrefu, kwa hiyo kwenye dirisha dogo kwa mapendekezo ya kocha tutatafuta mchezaji kuchukua nafasi yake japo CAF wameruhusu kusajili wachezaji 10 kwa ajili ya CAF Champions League"
"Tunaomba TFF watupe mwongozo kama tutaruhusiwa kusajili wachezaji 10 wa kimataifa," alisema Mo