Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji leo amekata mzizi wa fitina baada ya kutangaza kuwa wamemuongeza mkataba wa miaka miwili na nusu kiungo Mzambia Clatous Chama
Siku za karibuni kumekuwa na tetesi nyingi zinazomuhusu Chama akihusishwa na klabu ya Yanga
Akizungumza na Wanahabari mapema leo, Mo amesema wamemalizana na Chama
"Simba tumejipanga. Chama hajaenda popote, tumeshasaini nae mkataba na atabaki na Simba. Tumemalizana na Chama na ni mchezaji wa Simba kwa miaka miwili na nusu ijayo," alisema Mo
"" Tulikuwa tunataka tusiseme ili tumtangaze rasmi, sasa wenzetu wanafanya Propaganda, alafu unajua mashabiki, mtu yupo Mwanza, Singida Mwanasimba anaanza kupata ugonjwa wa moyo sasa hizi propaganda ya uongo sikubaliani nazo"
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Chama ni kama amethibitisha kumalizana na Simba kwa kuweka ujumbe ambao aliwaachia machabiki wamalizie : 'Once wa Lion'............Always wa Lion
Aidha Mo pia amekanusha tetesi zilizokuwa zikimuhusisha kiungo wa Yanga Mukoko Tonombe kutakiwa na Simba
""Suala la Kumsajili kiungo Mukoko ni propaganda tu na wala hatuja zungumzia hili suala kwenye bodi yetu""