James Kotei, vipi arudi au asakwe mwingine?

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Nov 2020
James Kotei, vipi arudi au asakwe mwingine?

Kiungo raia wa Brazil Gerson Fraga atakuwa nje kwa zaidi ya miezi sita baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Biashara United

Fraga aliongeza mkataba wa mwaka mmoja mwanzoni mwa msimu lakini anaweza asipate tena nafasi ya kuichezea Simba baada ya uongozi kufikia nae makubaliano kumruhusu arejee Brazil ili akapate muda wa kutosha kupona majeraha

Simba inatarajiwa kutumia dirisha dogo la usajili kushusha kiungo mwingine mkabaji kuchukua nafasi yake

Kwa mara nyingine, jina la Mghana James Kotei limeibuka katika orodha ya nyota wanaoweza kutua Msimbazi

Kazi aliyofanya Simba imeendelea kubaki mioyoni mwa mashabiki, haishangazi kuona mara kwa mara ametajwa kurejea Msimbazi

Kotei ni mchezaji mwenye mapenzi na Simba, mara kadhaa mwenyewe ameweka wazi hilo

Kuna wakati alihusishwa kuwaniwa na Yanga kupitia kampuni ya GSM, hata hivyo 'alichomoa' akisisitiza kujiunga na Yanga ni sawa na kuwasaliti mashabiki wa Simba anaoheshimiana nao sana

Hata hivyo tangu alipoondoka Simba, Kotei hakuwa na mwendelezo mzuri wa kucheza mpira

Alisajiliwa na Kaizer Chiefs lakini hakuweza kupata nafasi ya kucheza hata mchezo mmoja mpaka pale alipofikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake miezi mitano tu tangu walipomsajili

Akaelekea kule nchini Belarus ambako pia hakudumu, alivunja mkataba baada ya miezi minne tu

Pengine Simba inapaswa kujiridhisha na kiwango chake kwanza kabla ya kufikiria kumpa mkataba kwani muda aliokaa nje ni mrefu kuliko muda aliocheza

Lakini kama watajiridhisha kuwa bado anao uwezo, Kotei anaweza kuwa mchezaji sahihi kuchukua nafasi ya Fraga

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’