Bado tuna nafasi Afcon - Ndayiragije

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Nov 2020
Bado tuna nafasi Afcon - Ndayiragije

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije amesema bado wana nafasi ya kufuzu kwa fainali za Afcon 2021 kama watafanya vizuri katika michezo mitatu iliyobaki

Jana Tanzania ilifungwa bao 1-0 na Tunisia katika mchezo uliopigwa nchini Tunisia, timu hizo zitarudiana jijini Dar es salaam Novemba 17 2020

Matokeo hayo yameifanya Tanzania ishike nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa kundi J lakini ikiwa na alama tatu sawa na Equitorial Guinea na Libya

Ndayiragije amesema wanaelekeza nguvu zao kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Tunisia kuhakikisha wanaibuka na ushindi

Amesema watafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa jana ili waweze kufanya vizuri

"Haukuwa mchezo mwepesi, tulikutana na wapinzani ambao wako imara lakini hata sisi tulicheza vizuri. Yapo maeneo ambayo hatukufanya vizuri, tunajipanga kusahihisha makosa ili tufanye vizuri katika mchezo utakaochezwa nyumbani," alisema

"Kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu nafikiri itakuwa faida kwetu. Tutahakikisha tunapata matokeo mazuri ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kufuzu"

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki 30,000 kuingia uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mchezo huo ambao utaamua mustakabali wa Tanzania kufuzu fainali za Afcon 2021

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’