Kiwango cha juu alichoonyesha kiraka Erasto Nyoni katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 kati ya Tunisia dhidi ya Tanzania, unaweza kuwa mtihani kwa kocha Sven Vandenbroeck kufanya mabadiliko katika safu yake ya ulinzi
Tangu kuanza kwa msimu huu, Nyoni hana nafasi katika kikosi cha kwanza Simba, lakini kwa hakika amedhihirisha bado uwezo anao
Katika mchezo huo ambao Tanzania ilikubali kipigo cha bao 1-0, Nyoni ndiye aliyekuwa kiongozi kwenye safu ya ulinzi akishirikiana vyema na Bakari Nondo Mwamnyeto
Kocha Etienne Ndayiragije alifanya uamuzi sahihi wa kumjumuisha kwenye kikosi chake licha ya ukosoaji aliokumbana nao baada ya kumuita
Lakini kwa shughuli aiyofanya jana, hakuna mtu atazungumza tena juu ya uwepo wake Stars
ADVERTISE HERE