Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Mbuyi Yondani amewataka washambuliaji Emmanuel Okwi na John Bocco wafunge mabao mengi kwenye mechi ya kesho Jumapili ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Gendarmerie.
Simba ambayo haijashiriki michuano ya Afrika tangu mwaka 2013, kesho itakuwa Uwanja wa Taifa itakaporejea anga zake katika mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya awali.
Yondani aliyekuwa mtamu katika kutupia wavuni enzi zake, amesema licha ya mechi za kimataifa kuwa ngumu, lakini Okwi na Bocco wanapaswa kufunga mabao ya kutosha yatakayowapa nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Alisema Wekundu wa Msimbazi sasa wamebadilika na wanaonesha dhamira ya mafanikio, hivyo anaamini mchezo wa kesho mashabiki watatoka uwanjani kwa furaha.
“Ukiwatazama kwa sasa mambo yao si mabaya, wameimarika hasa ushambuliaji wakiongozwa na Okwi na Bocco. Kwa hiyo hata Jumapili wajitahidi kufunga mengi kadiri inavyowezekana,†alisema Yondani.
“Niwashauri Simba waingie uwanjani kwa malengo huku wakitambua kiu ya mashabiki wao na Watanzania kwa ujumla ni kutaka kuona Simba inasonga mbele,†aliongeza.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE