Mlinda lango Aishi Manula leo ameibuka shujaa wa Tanzania baada ya kuokoa mipira mingi ya hatari langoni licha ya Stars kufungwa bao 1-0 na Tunisia katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za Afcon 2021
Bao pekee la Tunisia lilifungwa na Youssef Msakni kupitia mkwaju wa penati kwenye dakika ya 18
Ulikuwa ni mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi, Tunisia wakitawala huku Stars wakicheza kwa tahadhari wakiwa nyuma ya mpira kwa muda mwingi
Kama sio umahiri wa Manula pengine mambo yangekuwa mabaya zaidi
Ni matokeo ambayo sio mazuri kwa Stars kwani vijana wa Etienne Ndayiragije watalazimika kushinda mchezo wa marudiano ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 17
Ili kubaki kwenye kinyan'ganiro cha kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afcon 2021, Stars inapaswa kushinda mchezo huo