Chama amewakataa Yanga kweupee

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Nov 2020
Chama amewakataa Yanga kweupee

Kiungo Mzambia Clatous Chama amethibitisha kuwa amefanya mazungumzo na uongozi wa Simba na kama kila kitu kitaenda sawa, atasaini mkataba mpya

Aidha Mzambia huyo amesema pamoja na kuwa na ofa nyingi mkononi, ameipa Simba kipaumbele

"Nimefanya mazungumzo na viongozi juu ya kuongeza mkataba mpya. Yapo mahitaji nimeyaweka mezani kwa viongozi wangu. Naamini kila kitu kitaenda sawa na karibuni nitaongeza mkataba," alisema Chama ambaye kwa sasa yuko Zambia akiwa na majukumu ya timu ya Taifa

"Kwa Tanzania kipaumbele nimewapa waajiri wangu Simba, sifikirii kujiunga na timu nyingine yoyote na hata ikitokea hatukufikia makubaliano basi nitaangalia ofa nyingine kutoka nje ya nchi. Nina ofa kutoka Afrika Kusini na hata Arabuni"

Nae Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa wasiwe na wasiwasi kwani Chama hataondoka Msimbazi

"Tumezungumza na Chama, tuko katika hatua ya mwisho kabisa kukubaliana asaini mkataba mpya. Nadhani kila kitu kitawekwa hadharani karibuni.

"Simba ndio klabu kubwa nchini, malengo yetu ni makubwa pia, Chama hawezi kuondoka Simba akajiunge na Yanga. Kama mashabiki wa Yanga wanamsubiri Chama kwenye timu yao basi wajiandae kisaikolojia kwani watamshuhudia Msimbazi kwa muda mrefu zaidi," alisema Barbara

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
6h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
6h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
9h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’