Kiungo mkabaji raia wa Brazil Gerson Fraga aatakuwa nje kwa muda mrefu kuuguza majeraha ya goti aliyopata mwanzoni mwa msimu huu
Madaktari wa klabu ya Simba wameelezwa kuwa Fraga anaweza kuwa nje mpaka miezi sita kuweza kupona kabisa majeraha hayo
Uongozi wa Simba unakusudia kusaka mbadala wake kwenye usajili wa dirisha dogo ambao utafunguliwa Disemba 15
Fraga aliongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Simba lakini ni wazi kutokana na majeraha aliyopata, anaweza asionekane tena kwenye kikosi cha mabingwa hao wa soka nchini
ADVERTISE HERE