Kumekuwa na tetesi nyingi kumuhusu kiungo wa Simba Clatous Chama ambaye anahusishwa kuwaniwa na klabu ya Yanga
Mkataba wa Chama unamalizika mwishoni mwa msimu, ameshafanya mazungumzo na uongozi wa Simba ili aweze kuhuisha mkataba wake
Inaelezwa kikao cha mwisho kilifanyika Alhamisi iliyopita na makubaliano kufikiwa Chama ataongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa nchi
Mwamba huyo wa Lusaka ameelekea nchini Zambia kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa
Uongozi wa Simba umewahakikishia wapenzi, wanachama na mashabiki wake kuwa Chama ataendelea kubaki Msimbazi
Wiki hii habari kubwa katika Magazeti ni usajili wa Mzambia huyo ambapo imeelezwa kuwa GSM wamejitosa mazima wakitaka kumsajili kwa kile kinachoelezwa kutaka kulipa kisasi cha pigo walilopewa kwenye usajili wa Bernard Morrison
Afisa Habari na Msemaji wa Simba Haji Manara amewahakikishia Wanamsimbazi kuwa hakuna mchezaji Chama atakayesajiliwa na Yanga labda kiwe chama cha siasa