Moto ni ule ule Gendarmarie wasubiri kipigo tu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Feb 2018
Moto ni ule ule Gendarmarie wasubiri kipigo tu
Benchi la Ufundi pamoja na wachezaji wa timu ya Simba wameahidi kuhamishia makali ya Ligi Kuu Tanzania Bara watakapoikaribisha Gendarmarie kutoka Djibouti katika mechi ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayofanyika kesho kwenye Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema kuwa kila siku wanaiandaa timu yao kusaka matokeo mazuri na anaamini ushindi mfululizo walioupata kwenye ligi utawaongezea ari ya kupambana wachezaji wao.

Djuma alisema kila mchezaji aliyeko katika kikosi cha Simba anafahamu malengo ya timu hiyo ambayo ilikuwa nje ya mashindano ya kimataifa kwa muda mrefu.

Kocha huyo raia wa Burundi alisema kuwa katika programu za mazoezi wameiandaa timu hiyo kucheza mifumo tofauti na hii ni kwa lengo la kuwazidi mbinu wapinzani wao endapo mfumo wa kwanza utashindwa kuwapatia mabao.

"Ni mechi ngumu kama zile za ligi, tunataka kuhakikisha tunapambana na kumaliza kazi hapa nyumbani kabla ya kuwafuata kwao, tumepata nafasi ya kuona video zake na kujua maeneo ambayo wanayategemea kuendesha timu," alisema kocha huyo wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda.

Naye mshambuliaji tegemeo na aliye katika kiwango cha juu nchini Mganda, Emmanuel Okwi, alisema kila mechi kwao ni sawa na fainali na siku zote hawadharau timu pinzani.

"Kila siku huwa nawaza kuisaidia timu yangu iweze kupata ushindi katika kila mechi, tunahamishia nguvu zile zile kwenye mashindano ya kimataifa kwa sababu tunataka mafanikio pia msimu huu," alisema mshambuliaji huyo raia wa Uganda.

Aliongeza kuwa anawapongeza mashabiki wa Simba kwa kushirikiana nao kwa karibu kuanzia mwanzo wa msimu na kuwaahidi wataendelea kupambana hadi mechi ya mwisho.

Baada ya mchezo huo wa kesho, Simba ambao wanaongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu watasafiri kuelekea Shinyanga kuwafuata Mwadui FC katika mchezo wa utakaofanyika Alhamisi kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
1h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
1h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
7h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
1d ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’