Hesabu za Niyonzima kuelekea mchezo dhidi ya Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
10 Oct 2017
Hesabu za Niyonzima kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
Kiungo fundi wa Simba, Haruna Niyonzima anaamini kikosi cha Simba kina nafasi kubwa ya kushinda dhidi ya Yanga Oktoba 28.

Niyonzima raia wa Rwanda amesema kikosi chao kina nafasi ya kufanya vizuri katika mechi hiyo dhidi ya timu yake ya zamani ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Bara inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Oktoba 28 katika Uwanja wa Uhuru katika mchezo wa kwanza kukutana msimu huu wa Ligi Kuu Bara huku kila upande ukitarajia kukumbana na upinzani mkali.

Haruna Niyonzima anakutana kwa mara ya kwanza na timu yake hiyo ya zamani kwenye ligi baada ya mechi ya Ngao ya Jamii waliyocheza Agosti 23 ambapo Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti.

Niyonzima amesema kuwa, mchezo huo mara nyingi unakuwa mgumu na wa kiushindani lakini kwa upande wao wanajipanga kuweza kushinda mechi hiyo.

“Mechi ya Simba na Yanga mara nyingi inakuwa mechi ngumu na ni kubwa, hivyo kikubwa ni kuangalia ni jinsi gani tunaweza kujituma ili kufanikiwa kufanya vyema.

“Mara nyingi timu hizi zikikutana zinakuwa na ushindani wa hali ya juu tofauti na unavyocheza na timu nyingine, hivyo kunahitajika umakini wa hali ya juu, kwa upande wangu nimejipanga ili kuweza kushinda mchezo huo.

“Kwa sasa mimi siwezi kukizungumzia kiwango cha Yanga kwa kuwa kwa sasa nipo Simba, lakini ninachokiangalia ni ushindi tu,” alisema Niyonzima.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →