Kiungo wa Simba Clatous Chama ameitwa kujiunga na timu ya Taifa ya Zambia inayojiandaa kuikabili Botswana katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya Afcon 2021
Chama tayari ameondoka nchini akiungana na nyota wengine wa Simba Luis Miquissone, Joash Onyango na Meddie Kagere ambao wameitwa timu za Taifa Msumbiji, Kenya na Rwanda
Wachezaji 12 wa Simba wameitwa kuzitumikia timu zao za Taifa ambapo wachezaji nane wameitwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Nyota walioitwa Stars ni pamoja na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Said Ndemla na John Bocco
ADVERTISE HERE