Wafahamu wapinzani wa Simba, Plateau United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Nov 2020
Wafahamu wapinzani wa Simba, Plateau United

Plateau United ni mabingwa wa ligi kuu ya Nigeria msimu uliopita, wakitwaa taji mbele ya Enyimba wakinufaika na uamuzi wa Chama cha Soka Nigeria kufuta msimu kutokana na janga la corona

Timu hii ilianzishwa mwaka 1975, na walitwaa ubingwa wa Nigeria kwa mara ya kwanza mwaka 2017

Walipanda daraja kushiriki ligi kuu ya Nigeria msimu wa 2010-11 kisha wakateremka daraja msimu uliofuata

Walipanda tena msimu wa 2014-15 na msimu mmoja baadae wakashinda taji la ligi kuu ya Nigeria

Mwaka 2018 wakashiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza

Timu hii haina rekodi ya kutisha katika michuano mikubwa barani Afrika, huu ukiwa msimu wao wa pili kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa

Wananolewa na kocha mzawa, Kennedy Boboye

Wanakutana na Simba ambayo tayari ina uzoefu mkubwa wa kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa mwaka 2018 ikifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali

Ni rasmi kuwa mchezo wa kwanza utapigwa kule nchini Nigeria kati ya Novemba 27-29 na mchezo wa marudiano kupigwa Disemba 04-06 jijini Dar es salaam

Hii ni nafasi kwa Simba kusahihisha makosa ya msimu uliopita walipotolewa hatua ya awali na UD Songo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’