Droo ya hatua ya awali ya michuano ya vilabu barani Afrika inafanyika leo nchini Misri yalipo Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF)
Klabu ya Simba itaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya ligi ya mabingwa wakati Namungo Fc wao watashiriki michuano ya kombe la Shirikisho
Kulingana na viwango vya ubora vilivyotolewa na CAF hivi karibuni, Simba ina nafasi kubwa ya kuanzia ugenini mchezo wake wa kwanza kama ilivyokuwa msimu uliopita
Timu 68 zinashiriki ligi ya mabingwa msimu huu
Kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona, droo hiyo haitakuwa na shamrashamra, hakutakuwa na uwakilishi wa timu na itafanyika na kusimamiwa na kamati ya Utendaji ya CAF
Michezo ya kwanza ya hatua ya awali itapigwa kati ya 27-29 Novemba 2020 na mechi za pili kupigwa Disemba 04-06
Timu zitakazofuzu hatua ya awali, zitatinga raundi ya kwanza ambapo watakaoshinda raundi ya kwanza watatinga hatua ya makundi wakati wale watakaoshindwa wathamishiwa hatua ya mtoano kombe la Shirikisho