Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa wamoja kuhakikisha wanafanikisha kile walichokipanga msimu huu
Gonzalez amewataka Wanasimba wasiyumbishwe na matokeo ya mchezo dhidi ya Yanga jana, wajivunie ubora wa timu yao
"Jana haikua siku yetu, lakini tunajivunia kwa jinsi mlivyopambana. Nawaomba tusitoke kwenye reli na tusivunjike moyo. Ligi ni ndefu na sisi ndo wenye timu bora. Tupambane," aliandika Barbara katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Simba ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga jana katika mchezo ambao mabingwa hao watetezi walikuwa na kila sababu ya kuondoka na alama zote tatu
Bado ni mapema sana kukata tamaa kwani kuna michezo 24 inasubiri kuchezwa
Kwa sasa Simba inaelekeza nguvu zake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ambapo droo ya hatua ya awali inatarajiwa kufanyika kesho Jumatatu jijini Cairo, Misri