Hans Poppe ashtukia hujuma, ataka uchunguzi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Nov 2020
Hans Poppe ashtukia hujuma, ataka uchunguzi

Zacharia Hans Poppe mmoja wa wajumbe wa Kamati ya usajili ya klabu ya Simba ameeleza kutofurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na baadhi ya wachezaji katika mchezo dhidi ya Yanga uliopigwa jana uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika kwa sare ya bao 1-1

Akizungumza baada ya mchezo huo ambao uliishuhudia Simba ikisawazisha bao dakika za lala salama kupitia kwa beki Joash Onyango, Hans Poppe aliwataja wachezaji Clatous Chama, Luis Miquissone na Larry Bwalya kuwa walicheza chini ya kiwango

"Angalia viwango vya Bwalya na Luis (Miquissone), hivi huwa wanacheza vile kweli?. Hata Chama mliyemuona leo ndiye hucheza vile kweli? Angalia bao alilokosa dakika za mwishoni mpaka sasa hatuelewi ilikuwaje, akakosa. Nafikiri kuna haja ya kuzungumza nao na kufahamu ilikuwaje?," alisema Hans Poppe

Juzi kabla ya mchezo kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck alimtaja Chama kuwa mmoja wa wachezaji majeruhi na pengine angekosa mchezo huo dhidi ya Yanga

Jana Chama alipoa sana, ilikuwa dhahiri mwamba huyo wa Lusaka hakuwa katika kiwango chake na pengine ndio sababu Hans Poppe amemtilia mashaka

Ikumbukwe mpaka sasa Chama amegoma kuongeza mkataba mpya licha ya kuwa tayari uongozi umemuwekea ofa nono mezani

Bwalya alitolewa baada ya dakika 45 nafasi yake ikichukuliwa na Hassan Dilunga wakati Miquissone pamoja na kuwa hakuwa na mchezo mzuri sana, juhudi zake zilionekana uwanjani

Β 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’