Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema vijana wake walistahili kushinda mchezo wa leo dhidi ya Yanga kama sio maamuzi yaliyokuwa yakiegemea upande mmoja
Simba imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Yanga katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
"Pamoja na kuwa hatukushinda, nawapongeza wachezaji wangu kwa mchezo mzuri walioonyesha hasa kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri sana, tulikuwa taratibu lakini pia waamuzi walijaribu kutupunguza kasi . Sina hakika na pigo la penati, nitaangalia marudio"
"Kipindi cha pili tulidhihirisha uimara wetu, tulitawala dakika zote. Matokeo haya kwetu ni sawa na ushindi kutokana na mazingira ya mchezo yalivyokuwa," aliongeza Sven
"Hatukuwa na muda mrefu wa kupumzika kuelekea mchezo huu kama ilivyokuwa kwa wenzetu lakini tumecheza vizuri"