Simba imelazimishwa sare ya bao 1-1 na wapinzani wao wa jadi Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo
Bao la dakika ya 86 lililofungwa kwa kichwa na beki Joash Onyango, lilitosha kuihakikisha Simba alama moja muhimu katika mchezo ambao watajilaumu wenyewe kwa kushinwa kuibuka na ushindi kwani waliutawala kwa muda mwingi hasa kwenye kipindi cha pili
Bao la Yanga lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Michael Sarpong, penati hiyo ililalamikiwa vikali na wachezaji wa Simba na hata mashabiki kwani ilikuwa dhahiri Tuisila Kisinda alifanyiwa madhambi na Onyango nje ya 18 lakini mwamuzi akaweka 'tuta'


Hata hivyo juhudi zilionyeshwa na wachezaji kipindi cha pili, ulikuwa mchezo ambao walistahili kushinda lakini hata alama moja sio haba
Matokeo haya yanaiacha Simba katika nafasi ya tatu baada ya kufikisha alama 20