Pira VPN, pira biriani kama kawaida leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Nov 2020
Pira VPN, pira biriani kama kawaida leo

Mabingwa wa nchi Simba jioni ya leo watakuwa na nafasi ya kuendeleza umwamba dhidi ya wapinzani wao wa jadi Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Simba itaingia kwa Mkapa ikiwa na lengo moja tu, kupata ushindi utakaowasogeza juu ya msimamo wakipunguza tofauti ya alama dhidi ya wapinzani wao hao

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema wamefanya maandalizi mazuri, wachezaji wake wako tayari kuendeleza pale walipoishia mwishoni mwa msimu uliopita wakishinda mabao 4-1

Simba leo itamkosa mshambuliaji wake Meddie Kagere ambaye yuko nchini Rwanda akitibu majeraha aliyopata kwenye mchezo wa ligi kuu mwezi uliopita

Mwamba wa Lusaka Clatous Chotta Chama kama kawaida leo, ataendelea kuwavuruga, Mugalu pia atakuwa na dakika zake!

Wakati upande wa Yanga tambo zikiwa nyingi kwenye mitandao ya kijamii, kwa Simba shughuli huwa inamalizika uwanjani

Msemaji na Afisa habari wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi wakashuhudie 'pira VPN' litakalochanganywa na 'pira biriani'

Ni utamaduni wa Simba kuwapa burudani mashabiki wao zaidi katika michezo dhidi ya Yanga

Utamaduni huo utaendelezwa pale kwa Mkapa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’