Kocha mkuu wa timu ya Simba, Sven Vandenbroeck amethibitisha kuwa atakosa huduma za wachezaji wake nyota watatu wa kikosi cha kwanza katika mchezo wa kesho wa watani wa jadi dhidi ya Yanga utakaopigwa saa 11 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Sven amewataja Clatous Chama, Chris Mugalu na Medie Kagere kuwa hawatakuwa sehemu ya mchezo kutokana na kuwa majeruhi.
Chama na Mugalu walipata majeraha katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar ambao Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0 katika uwanja wa Uhuru wakati Kagere yeye alipata majeraha muda mrefu na yupo nchini Rwanda kwa sasa.
"Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri isipokuwa tutakosa huduma ya Chama, Mugalu na Kagere kutokana nakuwa majeruhi," amesema Sven
Akizungumzia maandalizi ya mchezo, Sven amesema lengo lao ni kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu
"Ni mchezo wa watani wa jadi lakini pia ni mchezo ambao tunapaswa kuwa makini zaidi ili kushinda na kupunguza alama ambazo wametuzidi.”