Sven azitaka alama sita za Yanga, Azam Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Nov 2020
Sven azitaka alama sita za Yanga, Azam Fc

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandebrock amesema ni lazima wahakikishe wanashinda michezo dhidi ya Yanga na Azam FC  ili kuwa juu yao katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu

Simba baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, imewasogelea wapinzani wake Azam na Yanga kwa tofauti ndogo ya pointi.

Sven amesema ili kutetea ubingwa wao kwa msimu wa nne mfululizo, ushindi wa mechi dhidi ya Yanga hapo kesho na baadae Azam Fc ni matokeo muhimu

"Kushinda kila kitu ni ngumu lakini tumebakiza pointi chache kulingana nao, tuna kila kitu mikononi mwetu muhimu ni kushinda mechi mbili za Yanga na Azam hapo sasa tunaweza kuanza kufikiria ubingwa" alisema Sven baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar juzi

Kesho Jumamosi, Wekundu hao wa Msimbazi wanatarajiwa kukutana na watani wao wa jadi Yanga katika mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini

Kuelekea mchezo huo, Sven amesema vijana wake wako sawa japo wapo baadhi ya wachezaji anahitaji kuwaangalia hali zao baada ya kupata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Shomari Kapombe na Clatous Chama ndio wachezaji ambao walipata changamoto ndogo ndogo katika mchezo uliopita

Hata hivyo Sven amesema nyota hao watakuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Yanga Jumamosi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’