Jana Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu ya Simba Haji Manara aliwataka mashabiki wa timu hiyo watakaokwenda kwenye uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo wa Yanga dhidi ya St Louis kutowazomea Yanga.
Kauli yake hiyo imepingwa vikali na mashabiki wa Simba na wale wa Yanga kila mmoja akiamini ni jambo lisilowezekana.
Kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na mjadala mkali kuhusu kauli hiyo ya Manara.
Kimsingi wengi wameipinga na kutaka kila timu 'ipambane na hali yake'.
Ukweli ni kwamba upinzani wa Simba na Yanga ni wa kihistoria wala haujaanza leo wala jana.
Ukifuatilia Historia za timu zote, utabaini kwa nini sio jambo jepesi kwa mashabiki wa Simba kuisapoti Yanga na hivyo hivyo kwa mashabiki wa Yanga.
Mwaka 1993 Simba ilitinga fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika na mchezo wa marudiano wa fainali ulipigwa kwenye dimba la Uhuru zamani ukiitwa uwanja wa Taifa.
Simba ilikuwa ikichuana na Stella Abidjan na ilihitaji ushindi kutwaa taji la washindi Afrika baada kupata sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Ivory Coast.
Hata hivyo kilichotokea, idadi kubwa ya mashabiki wa Yanga walifurika kwenye uwanja wa Uhuru kuishangilia Stella Abdjan ambayo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Boli Zozo.
Kwa tukio kama hilo haiwezi kuwa rahisi leo kwa mashabiki wa Simba kwenda kuishangilia Yanga kama ilivyo kwa mashabiki wa timu hiyo kuishangilia Simba.
Adui muombee njaa ndio msemo unaotumiwa na mashabiki wa timu hizo. Na hakuna namna jambo hilo litabadilika!

ADVERTISE HERE