Ni mwendo wa kuchinja tu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Nov 2020
Ni mwendo wa kuchinja tu

Mabingwa wa nchi Simba wameapa kuendeleza pale walipoishia mchezo uliopita dhidi ya watani zao Yanga ambapo walishinda mabao 4-1 uwanja wa Benjamin Mkapa

Ulikuwa mchezo wa nusu fainali kombe la FA, Simba ikitinga fainali na hatimaye kutwaa taji hilo

Kikosi cha Simba kinakachoshuka dimbani kesho hakitakuwa na mabadiliko makubwa zaidi ni kuongezeka kwa silaha zaidi kina Joash Onyango, Larry Bwalya na Chris Mugalu

Simba imerejea kwenye mstari baada ya kushinda mechi mbili mfululizo, wakifunga mabao saba

Ni mchezo ambao Simba inahitaji ushindi ili kuendelea kusogea juu ya msimamo wa ligi

Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia alama 19, alama nne pungufu ya Yanga inayoshika nafasi ya pili na alama sita pungufu ya Azam Fc inayoshika nafasi ya kwanza

Azam Fc imecheza mechi moja zaidi. Upo uwezekano mkubwa wa Simba kurejea kileleni mapema kama watashinda kesho kwani baada ya mchezo huo, mchezo wa Yanga unaofuata ni dhidi ya Azam Fc

Tiketi za mchezo huo zimeanza kuuzwa juzi ambapo Viingilio Mzunguko 7,000/-, Viti vya Orange 10,000/-, V.I.P C 15,000/-, V.I.P B 20,000/- na V.I.P A 30,000/-.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’